Ripoti inayodai kuwa aliyekuwa meneja wa Chelsea,Jose Mourinho aliiandika Manchester United barua yenye kurasa sita akielezea upungufu wa kocha wa Man United Louis van Gaal imetajwa kuwa "ajabu kabisa", anasema wakala wake, Jorge Mendes.
Jarida la Independent la Jumapili pia limedai Mourinho aliwasilisha "uchambuzi wa kisayansi" wa kikosi kizima cha Old Trafford katika kile kinachoitwa " barua ya upendo" kwa klabu hiyo.
United walizomewa na mashabiki wao wa nyumbani hapo jana Jumamosi baada ya kulazwa bao 1-0 dhidi ya Southampton.
Mourinho, 52, hana kazi haswa baada ya kutimuliwa na Chelsea katika wa Desemba kufuatia matokeo duni.
Mendes alisema dhana ya kuwa Mreno huyo aliandika barua hiyo ilikuwa "ujinga".
Katika taarifa fupi: Mendez alisema "hamuoni kuwa kocha mwenye hadhi kama ya Mourinho hawezi kujidunisha kwa kuandikia vilabu nyaraka za kuomba kazi ?''
Baada ya kichapo hicho Old Trafford, vijana wa Van Gaal walizomewa sana na mashabiki .
Kilichowaaudhi sana ni takwimu kuwa Manchester United ilijifurukuta na kushambulia lango la wapinzani wao mara moja pekee katika mechi hiyo.
Van Gaal alinukuliwa akikiri kuwa yeye pamoja na vijana wake hawakufanya vyema katika mechi hiyo na kuwa walistahili kubezwa na kutupiwa matusi makali na mashabiki.
United wako katika nafasi ya 5 katika jedwali la ligi kuu ya Uingereza ikiwa na jumla ya alama 37.
Timu hiyo inahitaji zaidi ya alama 5 ilikunusuru nafasi nne za kwanza zitakayoiwezesha kushiriki katika ligi ya mabingwa barani Ulaya.
Alama hizo 37 ni za chini zaidi katika hiztoria ya klabu hiyo maarufu duniani baada ya kucheza mechi 23.
BBC Swahili
0 comments:
Post a Comment
Want to comment? write down here