UBALOZI wa Ubelgiji nchini jana ulimpa viza mshindi wa tuzo ya Mchezaji Bora wa Afrika kwa wachezaji wa ndani, Mbwana Samatta, ili kujiunga na timu yake mpya ya K.R.C Genk, huku ikimtakia mafanikio mema katika masuala yake.
Samatta alitwaa tuzo hiyo usiku wa Alhamisi ya wiki iliyopita na kupewa dola za Kimarekani15,000 (sawa na shilingi milioni 32 za Tanzania), baada ya kuwashinda wenzake wawili Mualgeria, Baghdad Boundjah, anayekipiga katika
klabu ya Etoile du Sahel ya Tunisia na kipa machachari wa TP Mazembe ya Congo DR, Robert Kidiaba.
Nyota huyo Mtanzania aliisaidia timu yake ya TP Mazembe kutwaa Kombe la Klabu Bingwa Afrika, huku akiibuka mfungaji bora baada ya kufikisha mabao saba na sasa anatarajia kujiunga na Klabu ya K.R.C ya Genk kwa mkataba wa miaka miwili na nusu ukiwa na thamani ya dola za Kimarekani 550,000 sawa na shilingi bilioni 1 za Tanzania.
Chanzo cha habari karibu na Samatta kilithibitisha mchezaji huyo kupewa viza jana, huku ubalozi wa nchi hiyo ukimpa baraka ya kufanikiwa katika mazungumzo na timu hiyo.
“Suala la visa halikuwa nawasiwasi kabisa kwa Samatta, ndiyo maana haikuchukua muda mrefu kufanikisha,” kilisema
CAF Africa Award 2016 live; Announcement of The Best African Based Player of the year
Newspaper Review: CAF Awards, 2016 CHAN 07/01/16
Sports This Morning: Discussion On Glo CAF Awards 07/01/16
Mbwana Ally Samata Skills Dribbling Goals
Mbwana Samata aweka historia ktk soka la Africa
Mshambualiaji wa TP Mazembe ambaye ni raia wa Tanzania Mbwana Ally Samatta jana ameingárisha Tanzania baada ya kuchaguliwa kuwa Mchezaji bora wa kiume wa Afrika kwa mwaka 2016.
Samatta ambaye amezungumziwa kujiunga na KRC Genk ya Ubelgiji akitokea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, amefanikiwa kuweka historia ya kuwa Mtanzania wa kwanza na mchezaji wa kwanza toka nchi za afrika Mashariki kutwaa tuzo ya Mchezaji Bora wa Afrika.
Tuzo hizo zilizofanyika jana usiku nchini Nigeria katika jijini la Abuja, Samatta aliinuka kidedea na kuwabwagwa mlinda mlango wa TP Mazembe, Robert Kidiaba, raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na mshambuliaji raia wa Algeria anayechezea Etoile du Sahel ya Tunisa .
Katika safari yake nchini Nigeria Samatta aliambatana na Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Selestine Mwesigwa . Mshambuliaji huyo wa Taifa Stars aliifungia klabu yake ya TP Mazembe mabao saba sawa na mshambuliaji wa El Merrikh ya Sudan, Bakri Al-Madina, na kuibuka kinara wa mabao. Katika tuzo hizo Pierre-Emerick Aubameyang, raia wa Gabon anayechezea Borussia Dortmund ya Ujerumani alitangazwa Mwanasoka Bora wa Afrika 2015 . Nafasi ya tatu katika tuzo ya Mwanasoka Bora Afrika ilimwendea mshambuliaji wa Swansea City ya England raia wa Ghana, Andre Ayew.
Akizungumza baada ya kutangazwa mshindi, Samatta alisema: "Najivunia sana kushinda tuzo muhimu sana kiasi hiki. Najionea fahari na kuonea fahari taifa langu pia. Natoka taifa (Tanzania) ambalo si moja ya mataifa makubwa katika soka Afrika. Kutawazwa kuwa mchezaji bora Afrika, ni jambo kubwa sana kwangu."
Washindi wa tuzo mbalimbali za mwaka huu ni Victor Osimhen (chipukizi bora), Herve Renard (kocha bora), Bakary Gassama (refa bora), Ivory Coast (timu bora ya taifa), TP Mazembe (klabu bora), Cameroon (timu bora ya taifa ya wanawake), Oghenekaro Etebo (kipaji cha mwaka) na Gaëlle Enganamouit (mwanasoka bora wa kike).
Ingawa sherehe ya kutangaza washindi wa tuzo hizo zilifanyika usiku, Magazeti ya Tanzania yamehakikisha habari za ushindi huo zinatoka ili kuufahamisha ulimwengu juu ya furaha yao kama inavyoonekana hapo juu.