Pages

Friday, 3 June 2016

Tanzania yashuka nafasi saba viwango FIFA


TANZANIA imeshuka nafasi 7 katika viwango vya soka vinavyotolewa kila mwezi na Shirikisho la soka Duniani ‘FIFA’ huku Argentina ikiendelea kuongoza.

Mei mwaka huu Tanzania ilipanda hadi nafasi ya 129 kabla ya kuporomoka hadi nafasi ya 136, huku  Kenya ikishuka nafasi 13 kutoka nafasi ya 102 hadi 129 wakati Uganda ikibaki nafasi ya 72 katika viwango hivyo.

Orodha hiyo iliyotolewa jana na FIFA, ilionesha kuwa Uganda inaongoza ukanda wa Afrika Mashariki na kati ikifuatiwa na Rwanda iliyopo nafasi ya 103, Ethiopia 125, Sudan Kaskazini 128, Kenya, Tanzania na Sudan Kusini 157.

Pia orodha hiyo ilionesha nchi ya Ivory Coast inaongoza Afrika kwa kuwa nafasi ya 36, ikifuatiwa na Ghana iliyokuwa nafasi ya 37 na Senegal iliyoko nafasi ya 41.

FIFA ilitaja Argentina kuwa kinara wa viwango vya soka duniani ikifuatiwa na Ubelgiji na Colombia huku nchi ya Tonga, Somalia na Eritrea zikiwa za mwisho kwenye orodha hiyo.

Na Adam Mkwepu, Mtanzania

Related Posts:

  • Bao la Samatta laibana Chad, Kenya yachapwa Bao la Mshambulizi wa Taifa Stars lilitosha kuipa Tanzania ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Chad katika mechi ya kufuzu kwa kombe la mataifa ya Afrika. Mkwaju wa Samatta kunako dakika ya 30 ya kipindi cha kwanza ilitosh… Read More
  • Ubora, udhaifu Yanga, Azam kimataifa Dar es salaam. Wakati Yanga na Azam zikijiandaa kukabiliana na vigogo vya soka Afrika kutoka kaskazini mwa bara hilo mwezi ujao, timu hizo zitabebwa au hata kuangushwa na washambuliaji, safu zao za ulinzi zinazohit… Read More
  • Michezo ya kufuzu Afcon kuendelea Kikosi cha Taifa la Ghana Michezo ya kusaka tiketi ya kushiki michuano ya kombe la mataifa ya afrika mwaka 2017 itayofanyika Gabon itaendelea tena leo Katika kundi A timu ya taifa ya Djibout itakua nyumbani katika uwan… Read More
  • Zlatan Ibrahimovic confirms Premier League interest ahead of potential summer move The Swedish strike ace is out of contract at French side Paris Saint-Germain this summer and has been tipped for a final fling in England Zlatan Ibrahimovic has admitted he is considering offers to move to the Premie… Read More
  • Samatta aibeba Genk Dar es Salaam. Mshambuliaji wa Kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta amefunga bao lake la kwanza Ulaya wakati timu yake Genk ikichapa Club Brugge kwa mabao 3-2 katika Ligi Kuu Ubelgiji. Samatta aliyeingia akitoke… Read More

0 comments:

Post a Comment

Want to comment? write down here