Pages

Saturday, 2 January 2016

Yanga kunoa makali Kombe la Mapinduzi


TIMU ya Yanga tayari imewasili Zanzibar kwa ajili ya kushiriki michuano ya Kombe la Mapinduzi itakayoanza kesho huku wakitamba kutwaa ubingwa na kusaka makali kwa ajili ya michuano ya Klabu Bingwa Afrika.

Katika mashindano ya Mapinduzi, Yanga imepangwa kundi B ikiwa na Azam, Mtibwa Sugar na Mafunzo ya Zanzibar ambapo inatarajia kufungua dimba kesho kwa kuvaana na Mafunzo.

Kikosi hicho kinachonolewa na kocha Hans Vans Pluijm na msaidizi wake, Juma Mwambusi, tayari kipo visiwani Zanzibar.

Katika misimu ya hivi karibuni, Yanga wamekuwa wakilalamikiwa kutokana na kupeleka kikosi B lakini msimu huu wameamua kutuma kikosi kamili wakiwa na malengo ya kutwaa ubingwa pamoja na kuongeza ujuzi kwa ajili ya michuano ya Klabu Bingwa Afrika.

Akizungumza kabla ya kuelekea Zanzibar, kocha Pluijm alisema kutokana na ugumu wa kundi walilopo ana imani kubwa utatoa changamoto kwa wachezaji wake ambao bado wana kazi kubwa ya kuhakikisha wanatetea ubingwa wa Tanzania Bara pamoja na kufanya vizuri katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika.

“Kikosi changu kamili kitakuwa Zanzibar na kila mchezaji atapangwa kulingana na uwezo wake atakaoonyesha kwenye mazoezi na baadhi ya mechi nimepanga kuwatumia wote kwani bado nina kazi kubwa mbele yangu.

“Nafikiri mashindano ya Mapinduzi yataongeza hali ya kimchezo kwa wachezaji wangu, kupitia mashindano hayo nitapata nafasi ya kuangalia mapungufu na kuyafanyia kazi na hii ni baada ya kukutana na timu ambazo hatujazizoea,” alisema.

Alisema baada ya Kombe la Mapinduzi kikosi chake kina kazi kubwa ya kujijenga ili kiweze kufanya vizuri katika kukabiliana na wapinzani wao, Cercle de Joachim ya Mauritius kwenye hatua ya kwanza ya mtoano wa michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika.

 NA ZAINAB IDDY, MTANZANIA

Related Posts:

  • Mayanja aanza vizuri na Simba Kocha Jackson Mayanja ameanza vyema kibarua chake Simba, baada ya kuiongoza timu hiyo kuichapa Mtibwa Sugar bao 1-0 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Mshambuliaji Hamis Kiiza aliifungia Simba bao hilo pekee kati… Read More
  • Samatta kuvuta mawakala wengi Tanzania BILA shaka kila mtu alisikia mshambuliaji wa TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na timu ya Taifa ya Tanzania, Mbwana Samatta alishinda tuzo ya mchezaji bora wa Afrika kwa wachezaji wa ndani. Ushindi wa… Read More
  • Ubelgiji wampa viza Samatta Kikwete ampongeza, amtaka acheze Ulaya UBALOZI wa Ubelgiji nchini jana ulimpa viza mshindi wa tuzo ya Mchezaji Bora wa Afrika kwa wachezaji wa ndani, Mbwana Samatta, ili kujiunga na timu yake mpya ya K.R.C Gen… Read More
  • Simba yavunja Mkataba na Makocha wake Simba sports club Dar es salaam 12-1-2016 Taarifa kwa vyombo vya habari Kwa masikitiko makubwa klabu ya Simba inawaarifu umma kupitia vyombo vya habari uamuzi wake wa kuvunja mikataba yake na makocha wake kocha … Read More
  • Yanga yatinga nusu fainali Mapinduzi Cup Mabingwa wa Tanzania Bara Timu ya Yanga, wamefanikiwa kutinga hatua ya Nusu fainali kufuatia ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mtibwa mabao ambayo yamefungwa na wachezaji Aboubakar na Malimi Busungu na kuwa kinara wa kundi … Read More

0 comments:

Post a Comment

Want to comment? write down here