Pages

Friday, 8 January 2016

Yanga yatinga nusu fainali Mapinduzi Cup


Mabingwa wa Tanzania Bara Timu ya Yanga, wamefanikiwa kutinga hatua ya Nusu fainali kufuatia ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mtibwa mabao ambayo yamefungwa na wachezaji Aboubakar na Malimi Busungu na kuwa kinara wa kundi B la michuano ya Kombe la Mapinduzi baada ya kujikusanyia jumla ya pointi 7.

Katika mchezo mwingine wa mapema wa kufuzu hatua ya nusu fainali, timu ya mafunzo imeichapa Azam FC 2-1 kwa ushindi usio na faida kwa timu hiyo baada ya kutupwa nje ya mashindano hayo kwa uchache wa pointi.

Yanga sasa watacheza nusu fainali na mshindi wa pili wa Kundi A huku Mtibwa Sugar nao wakikutana na mshindi wa kundi hilo.

Kundi A linamaliza mechi zake leo Ijumaa kwa Timu ya Jamhuri kuchuana na URA na Simba ikicheza na JKU huku kila timu ikiwa ina nafasi ya kutinga nusu fainali ikipata matokeo mazuri ingawa sare kwa Simba itawafikisha nusu fainali.

URA na Jamhuri zinahitaji ushindi.

Chanzo: BBC Swahili

Related Posts:

  • Yanga yarejea panapopendwa Mfungaji wa bao pekee la Yanga katika mchezo wa jana, Simon Msuva. TIMU ya soka ya Yanga jana ilimaliza mechi zake za viporo vyema kwa ushindi na kurejea kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara. Yanga iliibuka … Read More
  • Makocha watambiana ZIKIWA zimesalia siku tatu kabla ya pambano la watani wa jadi Simba na Yanga, makocha wa timu hizo wameonesha kuogopana huku kila mmoja akidai kuheshimu kikosi cha mwenziwe. Yanga imejichimbia Pemba na Simba imejichi… Read More
  • Yanga yatangaza raha WAWAKILISHI wa Tanzania Bara katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Yanga, leo wataikabili Cercle de Joachim ya Mauritius ukiwa ni mchezo wa marudiano hatua ya awali. Katika mchezo wa kwanza ugenini Uwanja wa Ge… Read More
  • Ubora, udhaifu Yanga, Azam kimataifa Dar es salaam. Wakati Yanga na Azam zikijiandaa kukabiliana na vigogo vya soka Afrika kutoka kaskazini mwa bara hilo mwezi ujao, timu hizo zitabebwa au hata kuangushwa na washambuliaji, safu zao za ulinzi zinazohit… Read More
  • Jonesia kuamua Simba na Yanga MWAMUZI Jonesia Rukiyaa wa mkoani Kagera, amepewa jukumu la kuchezesha mechi ya watani wa jadi Simba na Yanga, katika mchezo wao unaotarajiwa kuchezwa  Jumamosi hii Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Mwamuzi huyo m… Read More

0 comments:

Post a Comment

Want to comment? write down here