Simba sports club
Dar es salaam
12-1-2016
Taarifa kwa vyombo vya habari
Kwa masikitiko makubwa klabu ya Simba inawaarifu umma kupitia vyombo vya habari uamuzi wake wa kuvunja mikataba yake na makocha wake kocha mkuu Dylan Kerr na kocha wake wa makipa Iddi Salim.
Katika uamuzi wake uliofanywa mchana huu na kikao cha kamati ya utendaji ambapo makocha hao waliitwa klabu ya Simba na walimu hao kwa pamoja wamekubaliana kuvunja mikataba ya ajira zao kwa faida ya pande zote mbili.
Kwa sasa kocha msaidizi wa Simba Jackson Mayanja atakuwa na timu huku mchakato wa kumpata kocha mkuu ukiendelea..
Mwisho uongozi unawashukuru walimu hao kwa huduma waliyoitoa katika kipindi chote cha uwepo wao klabuni.
Imetolewa na Haji S.Manara
Mkuu wa mawasiliano wa klabu ya Simba.
Simba nguvu moja
0 comments:
Post a Comment
Want to comment? write down here