Pages

Sunday, 24 January 2016

Niyonzima rasmi Yanga


Sakata la Niyonzima kufukuzwa Yanga limechukua mwezi mmoja kabla ya wiki iliyopita kumalizana na kiungo huyo kuomba radhi ili aweze kurejeshwa kikosini.

Yanga ilitangaza kuvunja mkataba na Niyonzima kwa madai kwamba kwa kipindi kirefu mchezaji huyo amekuwa akifanya mambo na kuonyesha tabia ambazo si za kimichezo, gandamizi na ambazo zinaiathiri timu.

Ilidaiwa Niyonzima amekuwa akirudia mambo hayo, licha ya klabu kumuonya mara kadhaa kwa barua na wakati mwingine kumkata mshahara, lakini tabia zake zimekuwa zikiigharimu timu.

Pia ilidaiwa alikuwa akichelewa na kukosekana mara kwa mara katika programu za timu, hususan anapokuwa amekwenda likizo au kutumikia timu yake ya Taifa ya Rwanda, ambako mara zote amekuwa akiondoka bila hata klabu kupata taarifa au kuombwa ruhusa.

Lakini pia Yanga imemtuhumu Niyonzima kushiriki katika mashindano ambayo siyo rasmi na bila kuruhusiwa na klabu, akiweka maslahi yake mbele na si yale ya klabu.

Kutokana na mambo hayo, Yanga ilidai Niyonzima ameshindwa kuishi kwa kufuata vipengele vya mkataba wake kwa kushindwa kuthamini kazi yake na utovu wa nidhamu kwa programu za Yanga, hususan mazoezi ya maandalizi.

Hivyo basi, Yanga ilimtaka mchezaji huyo kulipa dola za Kimarekani 71,175 (sawa na Sh milioni 143) kama gharama za kuvunja mkataba na kwamba itapinga usajili wake popote bila kulipwa fedha hizo.
Lakini wiki iliyopita mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Bara walimalizana na mchezaji huyo ambapo aliomba msamaha na kurejeshwa katika timu.

Akizungumza baada ya kurudi katika kikosi hicho, Niyonzima alisema anajisikia furaha kurejeshwa kwenye timu na atatumia uwezo wake kusogeza Yanga mbele zaidi.

“Nashukuru kwa nafasi hii nyingine, naipenda sana Yanga, nafurahi kuungana na wenzangu tena. Hata kama kipindi niliposimamishwa niliendelea kuwasiliana na wenzangu kuwatia moyo na kuwakumbusha kuwa msimu huu tubebe ubingwa, kwani hiyo ndiyo heshima yetu pekee na kudhihirisha ubora wetu.

“Yalisemwa mengi, eti nina mapenzi na Simba, hapana si kweli, sasa nimerudi mashabiki wa Yanga wasubiri vitu zaidi, ni kawaida kupishana, nina imani hayatatokea tena,” alisema.


NA MSHAMU NGOJWIKE, DAR ES SALAAM
CHANZO : MTANZANIA

Related Posts:

  • Makocha watambiana ZIKIWA zimesalia siku tatu kabla ya pambano la watani wa jadi Simba na Yanga, makocha wa timu hizo wameonesha kuogopana huku kila mmoja akidai kuheshimu kikosi cha mwenziwe. Yanga imejichimbia Pemba na Simba imejichi… Read More
  • Mayanja asuka mkakati kuimaliza Yanga KOCHA wa Simba, Jackson Mayanja, amesema anaandaa mbinu mpya ili aweze kuifunga Yanga katika mchezo wao wa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara utakaochezwa Jumamosi hii katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. M… Read More
  • African Lyon yarejea Ligi Kuu Bara TIMU ya soka ya African Sports imerejea katika michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara licha ya kutoka sare ya bao 1-1 na Ashanti United, katika mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza (FDL) uliochezwa jana katika Uwanja wa Karume, … Read More
  • Yanga yatangaza raha WAWAKILISHI wa Tanzania Bara katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Yanga, leo wataikabili Cercle de Joachim ya Mauritius ukiwa ni mchezo wa marudiano hatua ya awali. Katika mchezo wa kwanza ugenini Uwanja wa Ge… Read More
  • Jonesia kuamua Simba na Yanga MWAMUZI Jonesia Rukiyaa wa mkoani Kagera, amepewa jukumu la kuchezesha mechi ya watani wa jadi Simba na Yanga, katika mchezo wao unaotarajiwa kuchezwa  Jumamosi hii Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Mwamuzi huyo m… Read More

0 comments:

Post a Comment

Want to comment? write down here