Kocha wa Mwadui FC ya Shinyanga, Jamhuri Kihwelo 'Julio'
Ushindi wa magoli 2-1walioupata Mwadui FC dhidi ya Ndanda FC umemtia kiburi kocha Jamuhuri Kiwhelo na kusema Simba wajiandae na kipigo kwenye mchezo wao wa Jumamosi.
Mwadui itaikaribisha Simba Jumamosi kwenye uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga huku Julio akikabiliana na waajiri wake wa zamani.
Akizungumza na gazeti hili jana, Julio alisema ushindi dhidi ya Ndanda ni salamu kwa Simba ambayo ameilezea kuwa imepoteza makali yake ya miaka ya nyuma.
“Timu yangu ipo vizuri na ushindi dhidi ya Ndanda ni salamu tu, tunawasubiri Simba na wao watapata kile walichokipata Ndanda.
“Ninakiandaa kikosi changu vizuri na sitegemei upinzani mkubwa kwa sababu Simba imepoteza makali yake,” alisema Julio.
Alisema, kuwa anafahamu Simba watataka kushinda mchezo huo haswa baada ya kubanwa mbavu na Toto African katika mchezo uliopita lakini watakutana na mlima kwenye uwanja wa Kambarage.
Endapo Mwadui itafanikiwa kushinda kwenye mchezo huo itafikisha pointi 24 na hivyo kuishusha Simba yenye pointi 23 mpaka nafasi ya tano na yenyewe ikitoka nafasi hiyo na kupanda mpaka nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi kuu.
NA RENATHA MSUNGU
CHANZO: NIPASHE
CHANZO: NIPASHE
0 comments:
Post a Comment
Want to comment? write down here