Pages

Sunday, 27 December 2015

LVG : Naweza kuondoka mwenyewe Man United


Kocha wa Manchester United Louis van Gaal amesema kuwa anaweza "kujiuzulu mwenyewe" baada ya Stoke City kuwapiga magoli 2-0 katika kichapo chao cha nne mfululizo katika michuano yote.

Mholanzi huyo, ambaye anakabiliwa na shinikizo baada ya kusajili mechi saba sasa bila ushindi, aliulizwa katika mahojiano na waandishi wa habari baada ya mechi iwapo ''anahofia kibarua chake kitaota nyasi ?''

Van Gaal, 64, alijibu kuwa hjilo lilikuwa jambo analostahili kujibu katika mazungumzo na mkurugenzi wa klabu hiyo Ed Woodward na si vyombo vya habari.

"Si siku zote ambapo ni klabu ndiyo inauwezo wa kufurusha kocha la ''

"Wakati mwingine mimi mwenyewe naweza kuchukua jukumu hilo mwenywe na kuhusiana na hilo sharti niende nifanye mkutano na mamlaka inayosimamia Manchester United safu yangu ya ukufunzi na kisha wachezaji wangu wala sio waandishi wa habari'' alifoka van Gaal.

United imekuwa na msururu wa matokeo duni uliosababisha Red Deivls wakatupwa nje ya Ligi ya Mabingwa katika hatua ya makundi mbali na kuporomoka kutoka kwenye orodha ya nne bora katika jedwali la ligi kuu ya Uingereza.

Van Gaal, aliyechukua nafasi ya David Moyes katika msimu wa 2014, alisema klabu hiyo alimuunga mkono siku zote ila aliongeza: "Tumepoteza hivyo kuna hali mpya.

"Nahisi msaada wa wachezaji wangu na bodi yangu.

Hata hivyo mashabiki wataudhika lakini hiyo inatarajiwa baada ya kushindwa mara nne .

" Van Gaal hafikiri ni muhimu kwamba Woodward haja muunga mkono hadharani .

"Kwangu mimi ni muhimu zaidi kwamba watu wanasema nini kuhusu utendaji kazi wangu " alisema. "Mimi sina haja sana na matamshi ya umma."

BBC Swahili

0 comments:

Post a Comment

Want to comment? write down here