Pages

Sunday, 3 January 2016

Pellegrini: Aguero atarudi kutamba


Meneja wa Manchester City Manuel Pellegrini ameeleza matumaini yake kwamba Sergio Aguero ataanza kufunga tena mabao.

Mshambuliaji huyo wa miaka 27 kutoka Argentina aliwafungia City bao la ushindi wakati wa ushindi wao wa 2-1 dhidi ya Watford, uliowafanya kuwa alama tatu pekee nyuma ya Arsenal.
Ilikuwa mechi yake ya tatu baada ya kukaa nje kwa zaidi ya mwezi mmoja kutokana na majeraha.

"Nina uhakika kipindi hiki cha pili cha msimu tutashuhudia uchezaji wa Aguero ambao tumezoea,” alisema Pellegrini.

Anahitaji mechi mbili au tatu kurejelea uchezaji wake wa kawaida.

“Bao alilofunga leo ni muhimu sana kwake. Kabla ya kufunga, alikuwa amecheza vyema, kuliko mechi iliyotangulia.”

Bao hilo la Jumamosi ndilo lake la 10 mashindano yote msimu huu. Matano aliyafunga mechi moja Oktoba dhidi ya Newcastle, ambayo ilikuwa yake ya mwisho kabla ya kukaa nje wiki sita kutokana na majeraha.

Sergio Aguero bado ndiye mfungaji mabao bora wa City ligini akiwa na mabao manane kutoka kwa mechi 13 za msimu huu. Anafuatwa na Raheem Sterling na Yaya Toure waliofunga mabao matano.

Chanzo : BBC Swahili

0 comments:

Post a Comment

Want to comment? write down here