Kocha Mkuu wa Majimaji ya Songea, Kalimangonga `Kally’ Ongala
KOCHA Mkuu wa timu ya Majimaji ya Songea, Kalimangonga `Kally’ Ongala amesema timu yake imejiandaa kuifunga Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara utakaofanyika leo Uwanja wa Majimaji.
Akizungumza na gazeti hili jana kwa njia ya simu, Ongala alisema wachezaji wake watapambana sana kushinda mechi zao zote zilizobaki wakianza dhidi ya Coastal ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kukwepa janga la kushuka daraja.
“Wachezaji wote wako salama, hatuna majeruhi yeyote lakini mechi ya kesho (leo) ni mechi ngumu na tunahitaji kila mchezaji awe makini sana kwani haitakuwa mechi rahisi kwa sababu Coastal nayo iko katika hali mbaya, itahitaji kujikwamua,” alisema Ongala, kocha msaidizi wa zamani wa Azam FC.
Majimaji ipo katika nafasi ya 10 ikiwa na pointi 27 ilizovuna katika michezo wakati Coastal inaburuza mkia miongoni mwa timu 16, ikiwa na pointi 19 tu baada ya kucheza mechi 25.
Baada ya mchezo dhidi ya Coastal, Majimaji itasafiri hadi Mwanza kuumana na Toto African ya huko Jumatatu ijayo.
Habari Leo
0 comments:
Post a Comment
Want to comment? write down here