Pages

Monday, 8 February 2016

‘Simba Tunataka ubingwa’


BEKI na Nahodha Msaidizi wa Simba, Hassan Isihaka amesema kwa sasa wanafanya vizuri katika Ligi Kuu Bara na mpaka wapinzani wao waje kushtuka tayari watakuwa kwenye ubingwa.

Isihaka alisema kwa sasa Simba wanaota ubingwa tu, hakuna jambo jingfine na kusema kuwa kwa kipindi chote tangu ameanza kuichezea Simba miaka minne iliyopita, inamuuma kuukosa ubingwa na kinachomshangaza, walikuwa wanacheza vizuri ila waliangushwa na bahati.

“Imani yangu ni kwamba msimu huu tutawafuta machozi mashabiki wa Simba kutokana na namna tunavyopata matokeo mazuri tunavyoshinda, maana awali, tulikuwa kama hatuna bahati kila tulipopambana hali ilikuwa ngumu.” Isihaka alisema na kuongeza:“Binafsi ninachokiamini, kufanya kwetu vizuri kasi yetu ni hadi tuchukue ubingwa, kama unavyojua wengine tangu tujiunge, Simba haijawahi kuchukua ubingwa huu.” 

Kuhusu wapinzani wao Yanga na Azam, beki huyo wa kati alisema wala hawaangalii wanafanya nini, akili zao kufanya yao ili kutimiza lengo la kutwaa ubingwa tu

Mwanaspoti

0 comments:

Post a Comment

Want to comment? write down here