Pages

Wednesday, 17 February 2016

Makocha watambiana


ZIKIWA zimesalia siku tatu kabla ya pambano la watani wa jadi Simba na Yanga, makocha wa timu hizo wameonesha kuogopana huku kila mmoja akidai kuheshimu kikosi cha mwenziwe.

Yanga imejichimbia Pemba na Simba imejichimbia Morogoro kwa maandalizi ya mechi hiyo ya Jumamosi.

Akizungumza na gezeti hili jana, kocha wa Yanga Hans van Pluijm alisema anafahamu ugumu wa mechi, lakini yeye anaendelea na programu yake ya kusaka ushindi kama kawaida.

“Mimi nakiandaa kikosi changu kwa ushindi kama ilivyo kwenye mechi zote tunazocheza, siandai kikosi changu kwa vile nacheza na Simba, hapana… najua mimi ni bingwa mtetezi nitakutana na ushindani mkubwa lakini nia yangu ni kushinda bila kujali nacheza na nani,” alisema.

Mechi ya mwisho ya ligi ya Yanga ilikuwa dhidi ya JKT Ruvu, ambapo ilishinda mabao 4-0. Pluijm alisema lengo lake ni kuendelea na ushindi.

“Najua kwa sasa ligi ni ngumu sana, kila timu inataka kushinda hasa inapokutana na timu yetu (Yanga) naandaa kikosi changu kushinda, naiheshimu Simba lakini hiyo haifanyi nishindwe kuhakikisha timu yangu inashinda,” alisema.

Kwa upande wa kocha wa Simba, Jackson Mayanja alisema kikosi chake kimejipanga kushinda Jumamosi.

“Tutaingia uwanjani kusaka pointi tatu kama tunavyofanya kwenye mechi zote, mechi ya Yanga tunaichukulia kama ilivyo mechi nyingine yoyote kwenye ligi sasa pointi tatu ni lazima,” alisema.

Tangu kuwa chini ya Mayanja, Simba imekuwa ikipata mfululizo hali iliyorudisha morali kwa wcahezaji na wapenzi wake na kuamini kwamba inaweza kufanya vizuri zaidi na kutwaa ubingwa.

“Kitu kama morali ambacho sikukikuta kwa wachezaji wangu nilipoanza kuwafundisha sasa naona kimerejea na kila mmoja unamwona ana tamaa ya ushindi nami nataka hilo liendelee,” alisema. “Tumeshapanga mikakati yetu na nimewaambia wachezaji wangu kwamba tunacheza mechi ya Yanga sio kutaka kulipa kisasi bali kutaka kupata pointi tatu, na hilo ndilo litakalokuwa,” alisema.

Katika mzunguko wa kwanza timu hizo zilipokutana Yanga ilishinda mabao 2-0.

Habari Leo

Related Posts:

  • Mayanja asuka mkakati kuimaliza Yanga KOCHA wa Simba, Jackson Mayanja, amesema anaandaa mbinu mpya ili aweze kuifunga Yanga katika mchezo wao wa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara utakaochezwa Jumamosi hii katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. M… Read More
  • Simba yatakata TAIFA huku Yanga ikifungwa MKWAKWANI Simba leo imezidi kuwapa raha mashabiki wake baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 4 - 0 dhidi ya African Sports uwanja wa Taifa Dar es salaam, huku Yanga ikilala kwa mabao 2 - 0 mbele ya Coastal Union uwanja wa Mkwakwani … Read More
  • Makocha watambiana ZIKIWA zimesalia siku tatu kabla ya pambano la watani wa jadi Simba na Yanga, makocha wa timu hizo wameonesha kuogopana huku kila mmoja akidai kuheshimu kikosi cha mwenziwe. Yanga imejichimbia Pemba na Simba imejichi… Read More
  • Jonesia kuamua Simba na Yanga MWAMUZI Jonesia Rukiyaa wa mkoani Kagera, amepewa jukumu la kuchezesha mechi ya watani wa jadi Simba na Yanga, katika mchezo wao unaotarajiwa kuchezwa  Jumamosi hii Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Mwamuzi huyo m… Read More
  • Niyonzima rasmi Yanga Sakata la Niyonzima kufukuzwa Yanga limechukua mwezi mmoja kabla ya wiki iliyopita kumalizana na kiungo huyo kuomba radhi ili aweze kurejeshwa kikosini. Yanga ilitangaza kuvunja mkataba na Niyonzima kwa madai kwamba … Read More

0 comments:

Post a Comment

Want to comment? write down here