Zlatana Ibrahimovic na Edison Cavan (pichani juu) wakishangilia ushindi baada ya kuifungia timu yao bao la kwanza na la pili
Klabu ya Paris St-Germain ya Ufaransa jana ilijipatia ushindi dhidi ya Chelsea katika mechi ya moja ya mzunguko wa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya .
Siku ya jana ilikuwa mbaya kwa Chelsea na hadi mwisho wa mchezo waliishia kuchezea kichapo cha mabao 2-1 .
Paris St-Germain walikuwa wa kwanza kuliona goli la Chelsea katika dakika ya 39 kupitia mshambuliaji hatari wa Sweden Zlatan Ibrahimovic .
Kupitia Mikel Obi ndani ya dakika ya 45 Chelsea nao walifanikiwa kusawazisha lakini furaha yao ilizimwa katika dakika ya 78 baada ya Edison Cavan kuongeza bao la pili bao ambalo lilidumu hadi mwisho wa mchezo na kuwafanya PSG wawe washindi kwa mechi ya jana.
Picha : Mirror
Picha zaidi kuhusu mechi hii fungu hapa
0 comments:
Post a Comment
Want to comment? write down here