Samatta akiwa katika vyumba vya kubailishia nguo vya timu yake mpya ya Grenk
Kocha bora wa michuano ya Kombe la Chalenji msimu uliopita, Adel Amrouche amesema mshambuliaji Mbwana Samatta ana nafasi ya kufanya vizuri akiwa Ubelgiji.
Samatta raia wa Tanzania, amejiunga na KRC Genk ya Ubelgiji akitokea TP Mazembe, siku chache baada ya kutangazwa mchezaji bora wa Afrika.
Amrouche raia wa Ubelgiji, aliyipa Kenya ubingwa wa Chalenji huku ikiwa na kikosi kinachoonekana hakina makali, amesema Samatta atafanya vizuri kama ataendelea kujiamini, lakini aongeze juhudi.
“Lazima aongeze juhudi, awe msikivu na asione tena kama yuko Afrika ambako alikuwa staa. Sasa ndiyo anaanza upya,” alisema Amrouche mwenye asili ya Algeria aliyewahi kuifundisha Motema Pembe ya Dr Congo.
Amrouche ambaye anasifika kwa kuwainua makocha vijana, alisisitiza Samatta ana kipaji na uwezo mkubwa. Lakini ushindani wa Ubelgiji unakuwa juu, lakini ataweza kupambana.
Tayari nahodha huyo wa timu ya soka ya Tanzania, Taifa Stars amecheza dakika 17 akiwa na kikosi cha Genk.
Salehe Jembe
0 comments:
Post a Comment
Want to comment? write down here