TIMU ya soka ya African Sports imerejea katika michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara licha ya kutoka sare ya bao 1-1 na Ashanti United, katika mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza (FDL) uliochezwa jana katika Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.
Matokeo hayo yameiwezesha timu hiyo kuongoza katika kundi A kutokana na pointi 29 walizojikusanyia huku Ashanti wakishika nafasi ya pili kwa kufikisha pointi 24.
Katika mchezo huo, African Lyon walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya tatu lililofungwa na Omary Abdallah kwa shuti kali.
Ashanti United walisawazisha dakika ya 50 kupitia kwa Mwini Ally ambaye alifanikiwa kuwatoka mabeki wa African Lyon na kuachia shuti lililojaa wavuni.
African Lyon imeungana na Ruvu Shooting kurejea Ligi Kuu baada ya kushuka daraja, huku Geita Gold ikipata nafasi ya kupanda daraja kwa mara ya kwanza baada ya kuongoza katika kundi C.
MSHAM NGOJWIKE/ MTANZANIA
0 comments:
Post a Comment
Want to comment? write down here