Pages

Sunday, 27 March 2016

CAF: Chad yajiondoa Tz mashakani


Chad imejiondoa kutoka kwenye kinyang'anyiro cha kufuzu kwa dimba la mataifa ya Afrika linalotarajiwa kufanyika mwakani huko Gabon.

Shirikisho la soka la Chad limefikia kauli hiyo kutokana na ukosefu wa fedha.

Katika barua iliyotumwa kwa shirikisho la soka la Tanzania,mwenyekiti wa shirikisho la soka la Chad Moctar Mahamoud, alisema kuwa hawana fedha za kutosha kufadhili safari ya kwenda Dar Salaam kwa mechi ya marudiano dhidi ya Taifa Stars hapo kesho.

CAF imewapiga marufuku Chad kutoka kwenye mashindano ya mwaka wa 2019 mbali na kuitoza faini ya dola $20,000 pesa za Marekani.

Kufuati kujiondoa kwa Chad sasa matokeo ya mechi zote dhidi ya Chad zimefutiliwa mbali na shirikisho la soka la Afrika CAF.

Chad ilikuwa inaburuta mkia katika kundi G.

Tanzania iliyokuwa imeratibiwa kucheza mechi ya marudiano dhidi ya Chad kesho sasa imesalia na pointi 1.

Misri iliyokuwa imeizaba Chad 5-1 sasa ndio wanaongoza kundi hilo wakiwa na alama 4.

Super Eagles ya Nigeria ambao wameratibiwa kuchuana dhidi ya Misri mjini Alexandria siku ya Jumanne sasa sharti washinde alama zote ilikumaliza katika nafasi ya kwanza.

Sheria za CAF zinasema kuwa endapo kundi litakuwa na timu 3 basi timu inayoongoza pekee ndiyo inayosonga mbele.

BBC Swahili

Related Posts:

  • I wouldn't sign for Chelsea right now - and nor would any top player, says Thierry Henry Sticking the boot in: Henry doesn't believe Chelsea will attract top talent this month The Blues are unlikely to qualify for next season's Champions League and it is not yet known who will manage the club when Guus Hid… Read More
  • Marseille yajitosa kumtaka Samatta Dar es Salaam. Wakati timu za Nantes na RCK Genk zikiendelea  kupigana vikumbo kwa ajili ya kuinasa saini ya mshambuliaji, Mbwana Samatta, klabu ya Olympique de Marseille nayo imejitosa kumuwania mshambuliaji huyo.… Read More
  • Simba yatakata TAIFA huku Yanga ikifungwa MKWAKWANI Simba leo imezidi kuwapa raha mashabiki wake baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 4 - 0 dhidi ya African Sports uwanja wa Taifa Dar es salaam, huku Yanga ikilala kwa mabao 2 - 0 mbele ya Coastal Union uwanja wa Mkwakwani … Read More
  • Niyonzima rasmi Yanga Sakata la Niyonzima kufukuzwa Yanga limechukua mwezi mmoja kabla ya wiki iliyopita kumalizana na kiungo huyo kuomba radhi ili aweze kurejeshwa kikosini. Yanga ilitangaza kuvunja mkataba na Niyonzima kwa madai kwamba … Read More
  • Mayanja aula mfupa uliomshinda Kerr Dar es Salaam . Kocha wa Simba, Jackson Mayanja ameamua kucheza kamali iliyomshinda mtangulizi wake Dylan Kerr kwa kuamua kuwapa nafasi wachezaji Rafael Kiongera na Hassan Isihaka katika kikosi chake cha kwanza. … Read More

0 comments:

Post a Comment

Want to comment? write down here