KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, Haruna Niyonzima amesema hana furaha kuwa nje ya Yanga na kuwataka mashabiki kuwa wavumilivu kwani suala lake linatarajiwa kupatiwa ufumbuzi hivi karibuni baada ya kuwasilisha maelezo yake kwa uongozi.
Akizungumza na gazeti la Habari leo juzi, Niyonzima alisema Yanga ni timu yake na ameishi nayo vizuri pamoja na watu wake hivyo anaamini tofauti zao zitamazilika na kurejea kuitumikia.
“Yanga ni timu yangu na nimeishi nayo vizuri pamoja na watu wake, lakini sina furaha kwani nimekaa nje kwa muda usiojulikana lakini haya yote ni majaribu na najua ni vitu ambavyo vipo duniani ila naamini yataisha vizuri tu,” alisema.
“Mimi ni binadamu naweza kufanya makosa lakini nawahakikishia wapenzi wa Yanga na wa Niyonzima kwamba hili litaisha siku si nyingi na wataendelea kupata burudani kama ilivyokuwa na zaidi”.
Pia aliwatakia heri Yanga kwenye mchezo wa leo na heri ya Krismasi na Mwaka Mpya 2016 na kuwataka wamalize mwaka 2015 kwa amani. Niyonzima amesimamishwa kwa muda usiojulikana na uongozi wa Yanga kutokana na kuchelewa kurudi kujiunga na timu hiyo baada ya kumalizika kwa mashindano ya Chalenji iliyofanyika Ethiopia ambapo yeye alikuwa akiitumikia timu yake ya taifa ya Rwanda.
0 comments:
Post a Comment
Want to comment? write down here