
TIMU ya Simba imethibitisha kushiriki michuano ya Kombe la Nile Basin Championship, itakayoanza Mei 22 mwaka huu nchini Sudan.
Katika mashindano hayo mwaka huu, bingwa atajinyakulia zawadi ya dola za Kimarekani 30,000 sawa na Sh 65,697,000 huku mshindi wa pili akizawadiwa dola 20,000 (sawa na Sh 43,798,000 wakati mshindi wa tatu akipata dola za Kimarekani 10,000 (sawa na Sh 21,899,000).
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Dar es Salaam...