Manchester City wameshinda Kombe la Capital One baada ya kuwashinda Liverpool kwenye fainali kupitia mikwaju ya penalti.
Willy Caballero ndiye aliyekuwa shujaa wa Manchester City, akiokoa mikwaju ya Lucas, Philippe Coutinho na Adam Lallana baada ya meneja Manuel Pellegrini kuwa na Imani naye na kumchezesha badala ya kipa nambari wani Joe Hart.
Manchester City walianza kwa kujiweka kifua mbele uwanjani Wembley kupitia bao la Fernandinho baada ya kosa la kipa wa Liverpool Simon Mignolet.
Mshambuliaji wa zamani wa Liverpool Raheem Sterling alipoteza nafasi wazi kabla ya Coutinho kusawazisha dakika za mwisho mwisho.
Mambo yaliisha sare 1-1.
Kwenye mikwaju ya penalti, Fernandinho aligonga mlingoti mkwaju wa kwanza wa City, lakini Jesus Navas na Sergio Aguero walifunga huku Caballero, 34, akiokoa mikwaju ya Liverpool na kutoa fursa kwa Yaya Toure kufungwa mkwaju wa ushindi.
Pellegrini alikuwa amebahatisha sana ikizingatiwa kwamba Caballero hakucheza vyema sana mechi waliyoshindwa 5-1 na Chelsea uwanjani Stamford Bridge raundi ya tano ya Kombe la FA.
Wengi wangetarajia amtumie Hart lakini aliamua kukwama na Caballero, ambaye walifanya kazi naye pamoja alipokuwa meneja Malaga.
Pellegrini ndiye aliyemnunua kipa huyo na kumpeleka Manchester.
Baada ya mechi, meneja wa Liverpool Jurgen Klopp alisema: "Tumevunjwa moyo sana lakini lazima tuinuke na kuendelea. Ni wajinga tu ndio husalia chini na kusubiri wachapwe tena.”
Kwa upande wake, Pellegrini alisema alisikitishwa sana na nafasi ambazo walipoteza muda wa kawaida wa mechi ingawa walicheza vyema muda wa ziada.
“Huu ni wakati muhimu sana kwetu, huwa muhimu sana kushinda kombe ukiwa Wembley."
BBC Swahili
0 comments:
Post a Comment
Want to comment? write down here