Droo ya raundi ya nne ya michuano ya kombe la FA imetoka huku timu za ligi kuu ya England zikipangwa na zile za daraja la chini.
Arsenal, ambao ni mabingwa watetezi wao wamepangwa kucheza na timu ya Burnley, Huku Chelsea wao wataanzia ugenini kwa kucheza na Mshindi wa mchezo kati ya Northampton Town au Mk Dons.
Man City wao watacheza na mshindi wa mchezo wa Wycombe Wanderers au Aston Villa. Huku majirani zao Man United wao watacheza na Derby County.
West Ham, wanasubiri mshindi wa mchezo unaowakutanisha Exeter City dhidi ya Liverpool.
Michezo hii ya raundi ya nne itachezwa January 29 mpaka Februari 1.
0 comments:
Post a Comment
Want to comment? write down here