Aliyekuwa kipa nambari moja wa timu ya Simba na Uganda Abel Dhaira ameaga dunia.
Dhaira mwenye umri wa miaka 28 alikuwa anaugua saratani.
Dr. Bernard Ogwel, wa shirikisho la soka nchini Uganda FUFA ameithibitishia BBC kuwa kipa huyo alivuta pumzi yake ya mwisho akiwa Iceland.
"Ni jambo la kuhuzunisha sana kuwa Dhaira ametuacha kwetu kama waganda na pia kwa Familia yake''
Dhaira alikuwa amejiunga na klabu ya IBV Vestmannaeyjar ya Iceland alipogunduliwa kuwa anaugua saratani katika miezi ya hivi karibuni.
Kipa huyo alianza kuichezea Uganda Cranes mwaka wa 2009 alipoisaidia timu hiyo kutwaa kombe la CECAFA Senior Challenge 2012.
Afya yake ilidhoofika Januari mwaka huu na akalazwa katika hospitali ya Nsambya kabla ya kurejea Iceland kwa matibabu zaidi.
Kocha wake wa IBV Vestmannaeyjar, Bjarni Johannsson alikuwa ameahidi kumsaidia kwa hali na mali wakati huu anapokabiliwa na maradhi.
Dhaira aliwahi kuichezea Express FC ya Uganda kabla ya kujiunga na AS Vita ya DR Congo na kisha Simba FC ya Tanzania.
BBC Swahili
0 comments:
Post a Comment
Want to comment? write down here