
Chad imejiondoa kutoka kwenye kinyang'anyiro cha kufuzu kwa dimba la mataifa ya Afrika linalotarajiwa kufanyika mwakani huko Gabon.
Shirikisho la soka la Chad limefikia kauli hiyo kutokana na ukosefu wa fedha.
Katika barua iliyotumwa kwa shirikisho la soka la Tanzania,mwenyekiti wa shirikisho la soka la Chad Moctar Mahamoud, alisema kuwa hawana fedha za kutosha kufadhili safari ya kwenda Dar Salaam kwa mechi ya marudiano dhidi ya Taifa...