Pages

Friday, 26 February 2016

Yanga yatangaza raha


WAWAKILISHI wa Tanzania Bara katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Yanga, leo wataikabili Cercle de Joachim ya Mauritius ukiwa ni mchezo wa marudiano hatua ya awali.

Katika mchezo wa kwanza ugenini Uwanja wa George V, Yanga ilishinda bao 1-0, matokeo ambayo yanawapa Yanga kazi nyepesi leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kutinga hatua inayofuata kwani inahitaji angalau sare.

Kocha wa Yanga, Mholanzi Hans van der Pluijm, amejitapa kushinda mchezo huo baada ya maandalizi mazuri waliyofanya kwa wiki mbili tangu warejee nchini.

Pluijm ambaye katika mchezo huo atawakosa nyota watatu wakiwemo wawili wa kimataifa, Haruna Niyonzima na mfungaji wa bao pekee lililowapa ushindi ugenini Donald Ngoma, alisema pamoja na kuhitaji sare, lakini lazima washinde.

“Tumejiandaa vizuri kuhakikisha tunashinda mchezo wa kesho (leo), kwa sababu tumefanya maandalizi ya kutosha na tunacheza nyumbani mbele ya mashabiki wetu hatutapenda kuwaangusha na kizuri zaidi tunawajua vizuri wapinzani wetu,”alisema Pluijm.

Pluijm alisema pamoja na kuwakosa nyota hao, lakini ana imani kubwa na wachezaji waliopo ambao ana hakika watacheza kwa kiwango cha juu na kuwapa ushindi. Wapinzania wa Yanga, Cercle de Joachim, tayari wametua Dar es Salaam kwa ajili ya mchezo huo huku wakionekana wamejipanga kuhakikisha wanalipa kisasi.

Kocha wa timu hiyo, Abdel ben Kacem, amesema amewajua vizuri Yanga na kwa maandalizi waliyoyafanya anaamini atafanikiwa kulipa kisasi. Katika hatua nyingine, kocha wa Simba, Jackson Mayanja, ameitabiria ushindi Yanga katika pambano la leo kwani wapinzani wao ni timu ambayo haina jina kubwa katika soka.

“Sitaki kuizungumzia sana Yanga, lakini nawapa nafasi kubwa ya kushinda mchezo huo, kwa sababu wana timu nzuri na tayari wana akiba ya bao kufuatia ushindi walioupata ugenini, lakini hata timu wanayocheza nayo ni dhaifu,” alisema Mayanja.

MOHAMED AKIDA/HABARI LEO

Related Posts:

  • Mayanja asuka mkakati kuimaliza Yanga KOCHA wa Simba, Jackson Mayanja, amesema anaandaa mbinu mpya ili aweze kuifunga Yanga katika mchezo wao wa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara utakaochezwa Jumamosi hii katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. M… Read More
  • Ubora, udhaifu Yanga, Azam kimataifa Dar es salaam. Wakati Yanga na Azam zikijiandaa kukabiliana na vigogo vya soka Afrika kutoka kaskazini mwa bara hilo mwezi ujao, timu hizo zitabebwa au hata kuangushwa na washambuliaji, safu zao za ulinzi zinazohit… Read More
  • Jonesia kuamua Simba na Yanga MWAMUZI Jonesia Rukiyaa wa mkoani Kagera, amepewa jukumu la kuchezesha mechi ya watani wa jadi Simba na Yanga, katika mchezo wao unaotarajiwa kuchezwa  Jumamosi hii Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Mwamuzi huyo m… Read More
  • Yanga yatangaza raha WAWAKILISHI wa Tanzania Bara katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Yanga, leo wataikabili Cercle de Joachim ya Mauritius ukiwa ni mchezo wa marudiano hatua ya awali. Katika mchezo wa kwanza ugenini Uwanja wa Ge… Read More
  • Makocha watambiana ZIKIWA zimesalia siku tatu kabla ya pambano la watani wa jadi Simba na Yanga, makocha wa timu hizo wameonesha kuogopana huku kila mmoja akidai kuheshimu kikosi cha mwenziwe. Yanga imejichimbia Pemba na Simba imejichi… Read More

0 comments:

Post a Comment

Want to comment? write down here