Pages

Thursday, 31 December 2015

Fifa kumwokoa Niyonzima


Dar es Salaam. Sakata la kuvunjwa kwa mkataba wa kiungo Haruna Niyonzima na klabu yake, Yanga limechukua sura mpya baada ya kuelezwa kuwa kwa mujibu wa kanuni za Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), mchezaji huyo anaruhusiwa kujiunga na timu yoyote na kuendelea kuitumikia kipindi hiki licha ya dirisha la usajili kufungwa.

Yanga juzi ilitangaza kuachana na Niyonzima kwa madai ya kukiuka mkataba wake, ikiwa zimepita siku 13 baada ya usajili wa dirisha dogo kufungwa. Aliyewahi kuwa Mkurugenzi wa Mashindano wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Saad Kawemba akifafanua sakata hilo alisema, Niyonzima ana haki ya kusajiliwa na klabu yoyote ya Ligi Kuu kipindi hiki na akaendelea kucheza kulingana na kanuni za Fifa.

“Mkataba unaweza kuvunjwa wakati wowote inategemea na masharti yaliyomo kwenye mkataba huo, katika soka kwa suala la Niyonzima, huyo ni mchezaji huru, hivyo kanuni za Fifa zinamruhusu kusajiliwa na klabu yoyote na akacheza hata kama dirisha la usajili limeshafungwa.

“Lakini, kwa hapa kwetu tunashindwa kufanya hivyo kutokana na weledi wa viongozi wetu na ikitokea inaweza kusababisha vurugu katika soka letu, lakini ili kuepusha hayo ni vyema kuheshimu mkataba na vipindi vya usajili,” alisema Kawemba.

Imani Makongoro / Mwananchi

0 comments:

Post a Comment

Want to comment? write down here