Liverpool wamepunguza kasi ya Leicester kileleni mwa Ligi ya Uingereza baada ya kuwalaza 1-0 uwanjani Anfield.
Leicester walikuwa wameenda mechi tisa bila kushindwa ligini na leo imekuwa mara yao ya kwanza kumaliza bila kufunga bao ligini msimu huu.
Uwanjani Britannia, masaibu ya meneja Louis Van Gaal yamezidi baada ya Red Devils kucharazwa 2-0 na Stoke City. Meneja huyo amekabiliwa na shinikizo baada ya klabu hiyo kuandikisha msururu wa matokeo mabaya.
Tottenham Hotspur nao wamefufua juhudi zao za kupigania taji la ligi kwa ushindi wa 3-0 dhidi ya Norwich City, wakisaidiwa sana na kipa Hugo Lloris anayesherehekea siku yake ya kuzaliwa leo.
Na uwanjani Stamford Bridge, hakukuwa na habari njema sana kwa kaimu meneja Guus Hiddink baada ya vijana wake wa Chelsea kutoka sare ya 2-2 na Watford.
Mshambuliaji wa Chelsea Diego Costa, aliyewafungia mabao yote mawili pia ameonyesha kadi ya manjano, hii ikiwa na maana kwamba hataweza kuwachezea dhidi ya Manchester United Jumatatu 28 Desemba.
Kiungo wao wa kati Oscar alipoteza nafasi nzuri ya kuwaweka kifua mbele alipoonekana kuteleza na kupoteza mkwaju wa penalti dakika za mwisho za mechi.
Kwa Manchester City uwanjani Etihad, ilikuwa siku ya mavuno, klabu hiyo ikipata ushindi wa 4-1 dhidi ya Sunderland licha ya Wilfried Bony kupoteza mkwaju wa penalti.
Man City ndio wenye nguvu zaidi - Pellegrini
Van Gaal aamini Man Utd watajinasua
19:52 Mechi zinamalizika
- Chelsea 2-2 Watford
- Bournemouth 0-0 Crystal Palace
- Liverpool 1-0 Leicester
- Man City 4-1 Sunderland
- Tottenham 3-0 Norwich
- Swansea 1-0 West Brom
- Aston Villa 1-1 West Ham
19:50 Jurgen Klopp anaingiza kiungo wa kati Lucas Leiva nafasi ya Philippe Coutinho. Liverpool bado wanaongoza 1-0 dhidi ya Leicester
19:46 Diego Costa anaonyeshwa kadi ya manjano. Hii ina maana kwamba atakosa mechi ya Jumatatu dhidi ya Manchester United uwanjani Old Trafford.
19:44 Mambo yalivyo EPL
- Aston Villa 1-1 West Ham
- Bournemouth 0-0 Crystal Palace
- Chelsea 2-2 Watford
- Liverpool 1-0 Leicester
- Man City 4-1 Sunderland
- Swansea 1-0 West Brom
- Tottenham 3-0 Norwich
Mechi ya awali:
Stoke 2-0 Man Utd
19:37 BAOOO! Tottenham 3-0 Norwich
Thomas Carroll anaongezea Spurs bao la tatu.
19:37 Chelsea 2-2 Watford
Chelsea wanapata penalti baada ya Hazard, aliyeingia nafasi ya Pedro, kuangushwa eneo la hatari. Oscar anajitokeza. Mkwaju wake unapaa juu na kukosa lango baada yake kuteleza.
19:32 Leicester wanapata nafasi nzuri lakini Mignolet anaokoa Liverpool.
19:27 Leicester wanafanya mabadiliko. Jamie Vardy anatoka na ndani anaingia Nathan Dyer, Leonardo Ulloa naye anaingia nafasi ya Shinji Okazaki.
19:25 Uwanjani Etihad, City wanapata penalti lakini mkwaju wa Wilfried Bony unapaa juu ya lango. Mambo bado ni City 4-1 Sunderland
19:23 BAOOO! Chelsea 2-2 Watford
Diego Costa anasawazishia Chelsea kwa bao lake la pili leo.
19:22 BAOOO! Aston Villa 1-1 West Ham
Jordan Ayew anasawazishia Villa.
19:20 BAOOOO! Liverpool 1-0 Leicester
Christian Benteke anafungia Liverpool.
19:16 BAOOO! Manchester City 4-1 Sunderland
Fabio Borini anakomboa bao moja upande wa Sunderland.
19:14 BAOOOO! Chelsea 1-2 Watford
Watford wanatwaa uongozi Stamford Bridge kupitia Odion Ighalo.
19:10 BAOOOO! Man City 4-0 Sunderland
De Bryune anafunga bao lake binafsi baada ya kuchangia sana katika ufungaji wa mabao hayo mengine.
19:00 Upande wa Swansea, bosi wao wa muda Alan Curtis anaingiza Jack Cork nafasi ya Jefferson Montero.
19:00 Chelsea wanamtoa Ces Fabregas na nafasi yake anaingia Jon Obi Mikel
19:00 Mechi zinaanza kwa kipindi cha pili
18:48 Ni wakati wa mapumziko sasa
18:45 BAOOO! Aston Villa 0-1 West Ham
Aaron Cresswell anafungia West Ham.
18:43 BAOOO! Chelsea 1-1 Watford
Troy Deeney anasawazishia Watford kupitia mkwaju wa penalti baada ya Nemanja Matic kunawa mpira eneo la hatari.
18:42 BAOOO! Tottenham 2-0 Norwich
Harry Kane anafungia Norwich la pili.
18:38 Divock Origi anaumia na kuondoka uwanjani upande wa Liverpool. Nafasi yake anaingia Benteke.
18:30 BAOOO! Chelsea 1-0 Watford
Diego Costa anafungia Chelsea bao la kwanza, baada ya kona kupigwa na Willian.
18:28 Jamie Vardy anapata nafasi kwenye lango upande wa Liverpool. Lakini mpira wake wa kichwa unapitia juu ya wavu.
18:26 BAOOO! Tottenham 1-0 Norwich
Harry Kane anafungwa kupitia mkwaju wa penalti ambayo imetolewa baada yake kuangushwa eneo la hatari.
18:24 Liverpool wanaendelea kushambulia Leicester. Divock Origi anapata nafasi nzuri lakini kipa anaunyaka mpira.
18:23 BAOOO! Manchester City 3-0 Sunderland
Wilfried Bony anaongezea City bao la tatu. Anafungwa kwa kichwa baada ya mkwaju wa adhabu kupigwa na Kevin de Bruyne.
18:18 BAOOO! Manchester City 2-0 Sunderland
Bao la Yaya Toure
18:14 BAOOO! Manchester City 1-0 Sunderland
City wanapata bao la kwanza kupitia Raheem Sterling ambaye amesaidiwa na Kevin De Bruyne
18:09 BAOOO! Swansea 1-0 West Brom
Swansea wanajiweka kifua mbele dhidi ya West Brom kupitia Ki Sung-yuen.
18:06 Liverpool wanashambulia Leicester, lakini kufikia sasa bado hakuna goli. Chelsea nao wameanza vyema lakini juhudi zao bado hazijazaa matunda.
18:00 Mechi zinaanza.
17:55 Kuhusu mechi iliyomalizika dakika chache zilizopita, kuna shabiki aliyefanikiwa kubashiri matokeo na hata wafungaji mabao siku sita zilizopita, 20 Desemba. Utabiri wake kuhusu Van Gaal utatimia?
17:50 Kwingineko, timu zimetangazwa kwa mechi zinazoanza saa kumi na mbili:
Liverpool Simon Mignolet analinda wavu badala ya Adam Bogdan, Divock Origi akiaminiwa na mashambulizi badala ya Christian Benteke.
Chelsea Gary Cahill anaingia nafasi ya Kurt Zouma anayewekwa kwenye benchi. Eden Hazard yuko benchi.
Manchester City, Sergio Aguero na Vincent Kompany wamerejea na wamo kwenye benchi.
Mechi zinazoanza ni:
- Aston Villa v West Ham 18:00
- Bournemouth v Crystal Palace 18:00
- Chelsea v Watford 18:00
- Liverpool v Leicester 18:00
- Man City v Sunderland 18:00
- Swansea v West Brom 18:00
- Tottenham v Norwich 18:00
17:36 Mechi inamalizika. Stoke City 2-0 Manccchester United
17:28 Anthony Martial anatoa kombora kulenga goli la Stoke. Kipa anautoa mpira nje na inakuwa kona.
17:26 Charlie Adam anapiga mpira wa mbali, hatua 35 kutoka kwenye goli. Unapaa juu ya wavu.
17:25 Andreas Pereira anaonyeshwa kadi ya manjano kwa kufanya madhambi.
17:20 Andreas Pereira anaingizwa nafasi ya Ander Herrera upande wa Man Utd.
17:09 Mame Biram Diouf anaingia nafasi ya Xherdan Shaqiri upande wa Stoke.
17:05 Marouane Fellaini anapata nafasi nzuri eneo la hatari baada ya kupata mpira kutoka kwa Rooney. Mpira wake unaokolewa na kipa.
17:03 Ashley Young anajaribu kupenyeza mpira, lakini Wayne Rooney ameotea.
16:52 Bojan wa Stoke anapewa kadi ya njano kwa kujiangusha.
16:50 Ander Herrera anashindia Man Utd frikiki.
16:49 Mchezo unaanza tena.
16:48 Kipindi cha pili. Van Gaal anamtoa Memphis Depay na kumuingiza nahodha Wayne Rooney. Upande wa Stoke, Marco Van Ginkel anaingia nafasi ya Glenn Whelan.
16:33 MAPUMZIKO Stoke City 2-0 Manchester United
16:31 Mata anatuma krosi nzuri eneo la hatari. Unatwaliwa na kipa.
16:25 Mechi inasimamishwa kwa muda. Marko Arnautovic wa Stoke anaonekana kuumia.
16:20 Arnautovic anapata nafasi nzuri. Anatoa kombora kali, lakini mpira unakosa wavu.
16:19 Pieters anaondoka uwanjani. Mechi inaanza tena.
16:18 Mechi inasimamishwa kwa muda. Erik Pieters anaonekana kuumia.
16:13 Man Utd wanapata nafasi eneo la hatari la Stoke. Fellaini anatoa kombora lakini tayari ameotea.
16:13 Man Utd wanashambulia. Ander Herrera anajishindia frikiki.
16:10 BAOOOO! Stoke City 2-0 Man Utd
Marko Arnautovic anafungia Stoke la pili.
16:09 Mpira wa Arnautovic unagonga mkono wa Ashley Young. Stoke wanapata frikiki.
16:04 BAOOOO! Stoke City 1-0 Manchester United
Bojan anafunga kwa guu la kulia baada ya kusaidiwa na Glen Johnson.
16:02 Mephis Depay anapata mpira eneo la hatari, lakini mpira wake unaenda moja kwa moja hadi mikononi mwa kipa wa Stoke.
15:56 Glenn Whelan anajishindia frikiki. Marko Arnautovic anapiga mkwaju lakini unakosa lango.
15:55 Manchester wanapata nafasi. Ander Herrera anapata mpira eneo la hatari na kutoa kombora ambalo linalenga goli. Kipa Jack Butland anaokoa.
15:50 Geoff Cameron anajaribu kupenyeza mpira, lakini Marko Arnautovic ameotea.
15:47 Marko Arnautovic anachomoka na kutoa pasi safi kwa Xherdan Shaqiri, krosi yake inapitia mbele ya goli. Stoke wanajikwamua na kupata kona. Lakini haizai matunda.
15:45 Mechi inaanza. Mata ananawa mpira.
15:40 Michael Carrick anaongoza wachezaji wa Utd kuingia uwanjani. Wachezaji sasa wanajiandaa kuanza mechi.
15:30 Wachezaji XI wa kuanza mechi ya Man Utd v Stoke City wametangazwa. Nahodha wa United Wayne Rooney amelishwa benchi. Michael Carrick ndiye atakayekuwa nahodha wa Utd leo
Manchester Utd XI: De Gea, Young, Jones, Smalling, Blind, Carrick, Herrera, Mata, Fellaini, Depay, Martial
Benchi: Rooney, Romero, Schneiderlin, Varela, McNair, Borthwick-Jackson, Pereira
Stoke City XI: Butland, Johnson, Shawcross, Wollscheid, Pieters, Cameron, Whelan, Shaqiri, Afellay, Arnautovic, Krkic. Benchi: Joselu, Wilson, Van Ginkel, Adam, Diouf, Walters, Haugaard.
15:29 Hujambo? Leo ni 26 Desemba, siku ya Boxing Dei na klabu zote EPL zinashuka dimbani Manchester United wakitangulia ugani Britannia huku kila timu ikipania kumaliza mwaka katika nafasi nzuri.
Karibu kwa matangazo ya moja kwa moja.
Mechi zinazochezwa leo ni kama ifuatavyo:
Mechi za Jumamosi 26 Desemba (Saa za Afrika Mashariki)
- Stoke v Man Utd 15:45
- Aston Villa v West Ham 18:00
- Bournemouth v Crystal Palace 18:00
- Chelsea v Watford 18:00
- Liverpool v Leicester 18:00
- Man City v Sunderland 18:00
- Swansea v West Brom 18:00
- Tottenham v Norwich 18:00
- Newcastle v Everton 20:30
- Southampton v Arsenal 22:45
BBC Swahili