Pages

Wednesday, 23 December 2015

Kocha Julio aitishia Simba

Kocha wa Mwadui FC ya Shinyanga, Jamhuri Kihwelo 'Julio'

Ushindi wa magoli 2-1walioupata Mwadui FC dhidi ya Ndanda FC umemtia kiburi kocha Jamuhuri Kiwhelo na kusema Simba wajiandae na kipigo kwenye mchezo wao wa Jumamosi.

Mwadui itaikaribisha Simba Jumamosi kwenye uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga huku Julio akikabiliana na waajiri wake wa zamani.
Akizungumza na gazeti hili jana, Julio alisema ushindi dhidi ya Ndanda ni salamu kwa Simba ambayo ameilezea kuwa imepoteza makali yake ya miaka ya nyuma.

“Timu yangu ipo vizuri na ushindi dhidi ya Ndanda ni salamu tu, tunawasubiri Simba na wao watapata kile walichokipata Ndanda.
“Ninakiandaa kikosi changu vizuri na sitegemei upinzani mkubwa kwa sababu Simba imepoteza makali yake,” alisema Julio.

Alisema, kuwa anafahamu Simba watataka kushinda mchezo huo haswa baada ya kubanwa mbavu na Toto African katika mchezo uliopita lakini watakutana na mlima kwenye uwanja wa Kambarage.

Endapo Mwadui itafanikiwa kushinda kwenye mchezo huo itafikisha pointi 24 na hivyo kuishusha Simba yenye pointi 23 mpaka nafasi ya tano na yenyewe ikitoka nafasi hiyo na kupanda mpaka nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi kuu.

NA RENATHA MSUNGU
CHANZO: NIPASHE

Mimi bado rais halali Fifa, adai Blatter


Zurich, Uswisi. Siku moja baada ya kufungiwa miaka minane, aliyekuwa rais wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), Sepp Blatter ameibuka na kueleza kuwa yeye bado ni kiongozi wa shirikisho hilo.

Alieleza kuwa haoni kosa lolote kiasi cha kumtia hatiani na kufungiwa miaka minane.

Alitetea malipo kwa swahiba wake, Michel Platini ambaye kwa pamoja wamefungiwa miaka minane.

Bosi huyo mwenye umri wa miaka 79 raia wa Uswisi alieleza kuwa ataendelea kuwa rais wa Fifa, hadi suala lake litakapoamuliwa na Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS) mjini Nyon.

Juzi, kamati ya maadili ya Fifa chini ya Jaji Hans-Joachim Eckert, raia wa Ujerumani iliamua kuwa fungia licha ya kuwasilisha pingamizi dhidi ya uamuzi huo.

Blatter alitiwa hatiani kwa kumlipa Platini, rais wa Shirikisho la Soka Ulaya (Uefa), Faranga za Uswisi 2 milioni (Pauni 1.35 milioni) mwaka 2011, ikiwa ni miaka tisa tangu wawili hao wadai kuwa na mkataba wa kazi ya ushauri ambayo ilistahili malipo hayo.

Mbali ya kufungiwa, Blatter alitozwa faini ya Faranga 50,000 au Pauni 34,000 na Platini, Faranga 80,000 au Pauni 54,000 kwa kosa hilo.

Akizungumza na wanahabari juzi mjini Zurich, Blatter akiwa na binti yake, Corinne alidai kuwa ameonewa.

“Kusema kwamba ni siku nzuri kwangu au Fifa, nitakuwa nimekosea,” alieleza Blatter.

“Huwezi kueleza kwamba mimi ni mtu anayetaka kujikosha. Mimi na mwanasheria wangu, tuliamini kuwa tumewaridhisha wanajopo, chini ya Jaji Eckert, tumewaeleza kila kitu kuhusu malipo. Tulifikiri kuwa kila kitu kilikuwa wazi.

“Tulikuwa na mkataba. Mkataba wa mwaka 1998 baada ya fainali za Kombe la Dunia. Kilichonishangaza ni uamuzi ambao umefikiwa dhidi yetu ambao haujazingatia makubaliano yaliyokuwapo. Mkataba huo ulithibitishwa na pande zinazohusika. Kulikuwa na ushahidi wa kufikiwa kwa makubaliano.

“Kwa hiyo, malipo hayo kwa Platini yalifanyika kulingana na kanuni za fedha kupitia kamati ya fedha, kamati tendaji kwa nia njema. Haikuwa hisani. Ni zawadi. Tuliepuka suala la rushwa. Tulifanya hivyo kulingana na kanuni za hesabu za Fifa.

“Unaweza kuwa na mkataba wa makubaliano ya mdomo. Safari ijayo, tutakwenda kwenye kamati ya rufaa. Ttutakwenda CAS,” alisema Blatter.

Kauli ya Platini
Naye Platini alidai kuwa atakwenda CAS ambako atakata rufaa kupinga uamuzi huo wa uonevu waliofanyiwa.

Alieleza kuwa dhamira yake ina amani. Alitaka hatua zichukuliwe kusafisha dhamira yake ambayo imechafuka.

Alieleza kuwa uamuzi huo unachafua sifa yake, unaua dhamira yake ya kugombea urais wa Fifa katika uchaguzi ujao.

Alisema kuwa alijua kuwa kamati hiyo isingeweza kuwatendea haki kwani kabla ya kumsikiliza Desemba 18 ilikuwa tayari imeamua adhabu.

Alisema uamuzi huo unalenga kumwondoa yeye katika ulimwengu wa soka. Blatter alitua mbele ya kamati ya maadili Alhamisi na kesho yake Platini alifika kwa ajili ya kujieleza ambako alieleza kuwa yeye alikuwa kama mpigania haki na marehemu Nelson Mandela aliyekuwa mtetezi wa haki, lakini hakupendwa na maadui zake kiasi cha kufungwa maisha jela.

Habari : Mwananchi
Picha: Kwa msaada wa Mtandao

Arsenal’s Mesut Ozil reveals the secret behind his sensational form... a good night’s sleep


MESUT OZIL has revealed the secret for his sensational form this season... a good night’s sleep.

The Arsenal ace, 27, has been on a hot-streak this season — and is already close to breaking Thierry Henry’s assist record of 20, on 15 already. And the German midfielder says it’s all down to a simple lifestyle change.

Ozil said: “The biggest change started when I was injured last year and I changed my diet and started to look at the small details in my life.

“For example I started to have physiotherapy on my days off and made sure I had a good sleep.

“That is crucial over here [in England]. It is the fastest league in the world and we often play twice a week with no winter break.”

And Arsenal will be hoping to clinch their first league title since 2003-04 on the back of Ozil’s form — sitting just two points of league leaders Leicester.

Wenger : Ushindi dhidi ya City umetupa tumaini


Meneja wa Arsenal Arsene wenger amefichua kuwa ushindi dhidi ya Man city imepiga jeki imani wanayohitaji katika mbio za kutwaa ligi ya Uingereza msimu huu.

Arsenal haijawahi kunyanyua taji hilo tangu mwaka wa 2004.

Hata hivyo mabao ya Theo Walcott na Olivier Giroud yalitosha dhidi ya Man City.

The Gunners walijifurukuta na kuwanyamazisha City mbele ya mashabiki wa nyumbani .

Licha ya bao la Yaya Toure Man city hawakuweza kuizima Gunners ambao walikuwa wakitafuta alama tatu muhimu na kupunguza pengo la alama kutoka kwa vinara wa ligi hiyo Leicester.

"Inatupa ujasiri, nguvu na," alisema Wenger, mwenye umri wa miaka 66.

"Kikosi kimeonyesha ukomavu ambao ungeweza kushuhudia katika mchuano tulipokuwa na shinikizo la kufanya vyema."
Arsenal inaoongoza city kwa alama 4 lakini bado wako alama mbili chini ya vinara Leicester City.

Huku mabingwa watetezi, Chelsea wakiwa nje ya mbio za kuwania taji la ligi, mababe hao wa kusini mwa London ndio wanaopigiwa upatu kuibuka washindi wa ligi.

Arsenal haijapoteza mechi 6 na ushidi wao katika mechi tano kati ya mechi zake sita umewawezesha kuchupa hadi nafasi ya pili msimu wa krismasi.

"Miaka miwili au mitatu iliyopita, tuliongoza kwa kipindi kirefu lakini uzuri wa wakati huu ni kuwa tumepoteza wachezaji bora, tulicheza dhidi ya Olympiakos, Villa na leo, tumeshinda mechi zote," alisema Wenger.

"Ni ishara nzuri. Naamini tumeonyesha uwezo wetu, matayarisho, na uhodari kwa jumla na imetupa alama tatu.

"Wakati tulikuwa tumechoka tulitegemea matumaini na hilo limetuwezesha tumalize katika nafasi nzuri."

Harakati za dakika za mwisho za City zilizoongozwa na Toure hazikutosha kuilemaza Arsenal.

City walionekana kupungukiwa ushupavu wao ugani Emirates bila beki wao wa kutegemewa, Vincent Kompany na Sergio Aguero aliyepata afueni baada ya kuuguza jeraha.

"Ilikuwa muhimu kwa Sergio kurudi kwa timu ,labda anahitaji mechi kadhaa kurejea katika fomu yake," alidai Pellegrini.

"Kuna alama 63 za kushindaniwa , mechi kadhaa na tulivyocheza katka kipindi cha pili inaonyesha tunazidi kushindania ligi."

City wamepoteza mechi tano msimu huu na timu ya mwisho kupoteza mechi tano kabla ya Krismasi na kushinda ligi ilikuwa Everton kati ya mwaka wa 1986-87.

Hata hivyo Pellegrini amesema kuwa; "Sijui takwimu lakini hatuko nje ya mbio za kushinda ligi. Ikiwa hauamini , hauko katika taaluma."

BBC Swahili