Pages

Friday, 8 January 2016

Yanga yatinga nusu fainali Mapinduzi Cup


Mabingwa wa Tanzania Bara Timu ya Yanga, wamefanikiwa kutinga hatua ya Nusu fainali kufuatia ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mtibwa mabao ambayo yamefungwa na wachezaji Aboubakar na Malimi Busungu na kuwa kinara wa kundi B la michuano ya Kombe la Mapinduzi baada ya kujikusanyia jumla ya pointi 7.

Katika mchezo mwingine wa mapema wa kufuzu hatua ya nusu fainali, timu ya mafunzo imeichapa Azam FC 2-1 kwa ushindi usio na faida kwa timu hiyo baada ya kutupwa nje ya mashindano hayo kwa uchache wa pointi.

Yanga sasa watacheza nusu fainali na mshindi wa pili wa Kundi A huku Mtibwa Sugar nao wakikutana na mshindi wa kundi hilo.

Kundi A linamaliza mechi zake leo Ijumaa kwa Timu ya Jamhuri kuchuana na URA na Simba ikicheza na JKU huku kila timu ikiwa ina nafasi ya kutinga nusu fainali ikipata matokeo mazuri ingawa sare kwa Simba itawafikisha nusu fainali.

URA na Jamhuri zinahitaji ushindi.

Chanzo: BBC Swahili

Mbwana SAMATA aingárisha Tanzania na kuwa Mchezaji bora wa Afrika kwa mwaka 2016



  
   

CAF Africa Award 2016 live; Announcement of The Best African Based Player of the year

Newspaper Review: CAF Awards, 2016 CHAN 07/01/16

Sports This Morning: Discussion On Glo CAF Awards 07/01/16

Mbwana Ally Samata Skills Dribbling Goals 

Mbwana Samata aweka historia ktk soka la Africa

Mshambualiaji wa TP Mazembe ambaye ni raia wa Tanzania  Mbwana Ally Samatta  jana ameingárisha Tanzania baada ya kuchaguliwa kuwa Mchezaji bora wa kiume wa Afrika kwa mwaka  2016.

Samatta ambaye amezungumziwa  kujiunga na KRC Genk ya Ubelgiji akitokea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, amefanikiwa kuweka historia ya kuwa Mtanzania wa kwanza na mchezaji wa kwanza toka nchi za afrika Mashariki kutwaa tuzo ya Mchezaji Bora wa Afrika.

Tuzo hizo zilizofanyika jana usiku nchini Nigeria katika jijini la Abuja,  Samatta aliinuka kidedea na kuwabwagwa mlinda mlango wa TP Mazembe, Robert Kidiaba, raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na mshambuliaji raia wa Algeria anayechezea Etoile du Sahel ya Tunisa .

Katika safari yake nchini  Nigeria Samatta   aliambatana na Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Selestine Mwesigwa . Mshambuliaji huyo wa Taifa Stars aliifungia klabu yake ya TP Mazembe mabao saba sawa na mshambuliaji wa El Merrikh ya Sudan, Bakri Al-Madina, na kuibuka kinara wa mabao.  Katika tuzo hizo Pierre-Emerick Aubameyang, raia wa Gabon anayechezea Borussia Dortmund ya Ujerumani alitangazwa Mwanasoka Bora wa Afrika 2015 . Nafasi ya tatu katika tuzo ya Mwanasoka Bora Afrika ilimwendea mshambuliaji wa Swansea City ya England raia wa Ghana, Andre Ayew.

Akizungumza baada ya kutangazwa mshindi, Samatta alisema: "Najivunia sana kushinda tuzo muhimu sana kiasi hiki. Najionea fahari na kuonea fahari taifa langu pia. Natoka taifa (Tanzania) ambalo si moja ya mataifa makubwa katika soka Afrika. Kutawazwa kuwa mchezaji bora Afrika, ni jambo kubwa sana kwangu."

Washindi wa tuzo mbalimbali za mwaka huu ni Victor Osimhen (chipukizi bora), Herve Renard (kocha bora), Bakary Gassama (refa bora), Ivory Coast (timu bora ya taifa), TP Mazembe (klabu bora), Cameroon (timu bora ya taifa ya wanawake), Oghenekaro Etebo (kipaji cha mwaka) na Gaëlle Enganamouit (mwanasoka bora wa kike).

Ingawa sherehe ya kutangaza washindi wa tuzo hizo zilifanyika usiku,  Magazeti ya Tanzania yamehakikisha habari za ushindi huo zinatoka ili kuufahamisha ulimwengu juu ya furaha yao kama inavyoonekana hapo juu.

Mwanasoka Bora Afrika

2015    Pierre-Emerick Aubameyang (Gabon)

2014    Yaya Toure (Ivory Coast)

2013    Yaya Toure (Ivory Coast)

2012    Yaya Toure (Ivory Coast)

2011    Yaya Toure (Ivory Coast)

2010    Samuel Eto’o (Cameroon)

2009    Didier Drogba (Ivory Coast)

2008    Emmanuel Adebayor (Togo)

2007    Frederic Kanoute (Mali)

2006    Didier Drogba (Ivory Coast)

2005    Samuel Eto’o (Cameroon)

2004    Samuel Eto’o (Cameroon)

2003    Samuel Eto’o (Cameroon)

2002    El Hadji Diouf (Senegal)

2001    El Hadji Diouf (Senegal)

2000    Patrick Mboma (Cameroon)

1999    Nwankwo Kanu (Nigeria)

1998    Mustapha Hadji (Morocco)

1997    Victor Ikpeba (Nigeria)

1996    Nwankwo Kanu (Nigeria)

1995    George Weah (Liberia)

1994    Emmanuel Amunike (Nigerua)

1993    Rashid Yekini (Nigeria)

1992    Abedi Pele (Ghana)

Mwanasoka Bora wa Afrika kwa Wachezaji wa Ndani

2015    Mbwana Samatta (Tanzania – TP Mazembe)

2014    Firmin Ndombe Mubele (DR Congo – Vita Club)

2013    Mohamed Aboutrika (Misri – Al-Ahly)

2012    Mohamed Aboutrika (Misri – Al-Ahly)

2011    Oussama Darragi (Tunisia – Espérance)

2010    Ahmed Hassan (Misri – Al-Ahly)

2009    Tresor Mputu (DR Congo – TP Mazembe)

2008    Mohamed Aboutrika (Misri – Al-Ahly)

2007    Amine Chermiti (Tunisia – Étoile du Sahel)

2006    Mohamed Aboutrika (Misri – Al-Ahly)

2005    Mohamed Barakat (Misri – Al-Ahly)


Angalia habari zinazomuhusu Mbwana Ally Samatha

Video na Picha : Kwa Msaada wa Mtandao

Sunday, 3 January 2016

Ngonjera za uwanja Simba zafikia patamu


Dar es Salaam. Ngonjera kuhusu ujenzi wa uwanja wa kisasa wa klabu ya Simba zimehamia mwaka 2016, huku ikielezwa kuwa tayari klabu hiyo imepata mwekezaji. Uwanja huo ulioko Bunju, nje kidogo ya Dar es Salaam umegeuka hekaya za viongozi wa klabu hiyo kwa muda mrefu sasa.

Jana, kiongozi mwandamizi wa klabu hiyo aliliambia gazeti hili kuwa wapo katika hatua za mwisho za kusaini mkataba na mwekezaji huyo mzawa kwa ajili ya kuanza ujenzi wa uwanja wao na ujenzi kupangwa kuanza rasmi mwishoni mwa mwezi.

Klabu hiyo, pia ilithibitisha kupata mwekezaji aliyetajwa kuwa ni Mtanzania na kwamba hadi kukamilika kwa uwanja huo utagharimu zaidi ya Sh2 bilioni.

Rais wa klabu hiyo, Evance Aveva hakuwa tayari kukubali wala kukanusha kufikiwa kwa hatua hiyo.

Awali, kiongozi huyo wa Simba alilithibitishia gazeti hili kuwa makubaliano baina ya pande hizo mbili yamefikia hatua nzuri.

Kiongozi huyo ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya utendaji ya klabu hiyo alisema mchakato wa kupata mwekezaji na ujenzi umefikia hatua ya makubaliano ambayo yako katika hatua za mwisho na wakati wowote mwezi huu ujenzi utaanza.

“Tayari, tumepata mwekezaji mzawa amekubali kujenga uwanja wetu na kwa kweli tuko katika hatua nzuri na niwaambie wapenzi na mashabiki wetu (Simba) hadi kufikia Januari 30, wataanza kuona mabadiliko kule Bunju,” alisema kiongozi huyo na kuongeza:
“Hadi kukamilika ramani yetu ya mwanzo ilionyesha tutatumia sh2bilioni, lakini huenda ikapungua au kuongezeka, itajulikana rasmi karibuni ni kiasi gani tutatumia, lakini awali ilikuwa Sh2 bilioni.”

Mohammed Dewji
Kuhusu uwekezaji wa mfanyabiashara maarufu, Mohamed Dewji (MO) ambaye amekuwa akitajwa kuitaka klabu hiyo , kiongozi huyo alisema suala lake halikuwa rasmi, bali mazungumzo ya pembeni.

“Mo hakuja rasmi kwetu, alikuwa akizungumza pembeni, hivyo, hatukuwa na sababu ya kusikiliza vitu ambavyo si rasmi, alibainisha kiongozi huyo.

Aveva alipoulizwa kuhusu MO, alisema aachwe apumzike kipindi hiki cha sikukuu.

Wakati huo huo, suala la kocha msaidizi wa timu yao, baada ya kuondoka kwa Seleman Matola, jukumu hilo limeachwa kwa kocha mkuu, Dylan Kerr.

Uongozi wa klabu hiyo umeeleza kutokuwa tayari kumwingilia kocha huyo na kusisitiza kuwa atakapokuwa tayari yeye ndiye ataupa uongozi taarifa za kocha aliyempata.

Ushindi wa juzi wa Simba dhidi ya Ndanda umempa Kerr aliyeuelezea kuwa umempa nguvu ya kutetea taji kwenye mashindano ya Kombe la Mapinduzi Zanzibar, ambako timu hiyo itakata utepe na Jamhuri ya Pemba kesho usiku.

Imani Makongoro/ Mwananchi

Sadio Mane aachwa nje kwa kuchelewa


Meneja wa Southampton Ronald Koeman amesema alimuweka nyota Sadio Mane kwenye benchi kwa sababu ya kuchelewa kufika kwa kikao cha kabla ya mechi.

Kiungo huyo wa kati wa Senegal aliwekwa kwenye benchi mechi ambayo klabu yake ililazwa 1-0 na Norwich Jumamosi, na alichezeshwa dakika 10 za mwisho pekee.

"Ni lazima uwaheshimu wachezaji wenzako, na mashabiki na klabu kwa sababu huwa inalipia pesa nyingi,” Koeman aliambia BBC Sport.

"Kunilazimisha kubadilisha kikosi saa mbili kabla ya mechi ni jambo lisilokubalika."

Sadio Mane, 23, alijiunga na klabu hiyo kutoka Red Bull Salzburg mwaka 2014, na alikuwa amewachezea mechi zote 19 Ligi ya Premia msimu huu, na kuwafungia mabao mara tatu.

"Hii ni mara ya pili tukio kama hili kufanyika. Mwaka jana kuna wakati alichelewa kufika uwanjani na leo alichelewa kufika kikao cha kabla ya mechi,” Koeman ameongeza.

“Siwezi kuelewa ni vipi makosa ya aina hii yanaweza kutokea.”

Kando na kumkosa Mane, Southampton waliathiriwa pia na kufukuzwa uwanjani kwa Mkenya Victor Wanyama, dakika mbili kabla ya Alex Tettey kufungia Norwich bao la ushindi mechi hiyo ya Jumamosi.

BBC Swahili

Niyonzima aitishia nyau Yanga


Dar es Salaam. Kiungo Haruna Niyonzima ameipa Yanga siku nne kubadili uamuzi wa kumfukuza na baada ya hapo ataanika ukweli wa mgogoro wake na klabu hiyo.

Wakati Niyonzima akisema hayo, katibu mkuu wa Yanga, Dk Jonas Tiboroha alisema jana kuwa pamoja na klabu hiyo kutompa rasmi barua ya kukatisha mkataba, uamuzi huo haujabadilika.

“Ni kweli hajapewa barua, inaandaliwa, atapewa wakati wowote na hivyo suala la kusema yeye bado ni mchezaji wetu anaweza kusema, hazuiwi,” alisema Tiboroha.

Kiungo huyo wa Rwanda alisisitiza kujua kinachoendelea juu yake ndani ya klabu hiyo na kueleza kuweka wazi kila kitu ndani ya siku nne.

Alisema hatambui kuachwa kwake, huku akisisitiza kuwa yeye bado ni mchezaji halali kwani bado hajapewa barua rasmi ya kuvunjiwa mkataba wake.

“Najua kinachoendelea, nilichopanga kukifanya nakijua, ingawa sitapenda kukiweka wazi sasa, ndani ya siku nne hadi Jumanne nitaweka wazi kila kitu juu ya mgogoro huo na hatma yangu kisoka,” alisema.

Aliongeza kuwa hivi sasa kila mtu anasema analojua kuhusu mgogoro wake na Yanga, lakini yeye ndiye anayejua kila kitu na kubainisha muda mwafaka ukifika hatakuwa na sababu ya kuficha ukweli zaidi ya kuweka wazi nini kinachoendelea.

“Sijali kwa kinachotokea, haya ni mapito, lakini ukweli naujua, nilikuwa kimya nikijipanga, lakini ndani ya siku nne nitaeleza ukweli wangu na Yanga na nini nitafanya,” alisema.

Alieleza kuwa anatambua kila kitu kinachoendelea ndani ya klabu hiyo, lakini muda mwafaka ukifika ataweka wazi siri hiyo ya moyo wake.

Kuhusu kurejea APR ya Rwanda, kiungo huyo mchezeshaji alisema kila kitu ni utaratibu, ingawa hawezi kulizungumzia jambo hilo kwani bado anajua yeye ni mwajiriwa halali wa Yanga na bado anatambua mkataba wake na klabu hiyo.

Niyonzima alitupiwa virago Yanga kwa kile kilichodaiwa kuwa ni kukiuka makubaliano ya mkataba baada ya nyota huyo kuchelewa kujiunga na wenzake alipomaliza kuitumikia timu yake ya taifa ya Rwanda, Amavubi kwenye mashindano ya Chalenji nchini Ethiopia

Imani Makongoro / Mwananchi