Pages

Friday 26 February 2016

Ox-lade Chamberlain hatacheza mpira kwa wiki kadhaa kutokana na kuumia goti






Kiungo machachari wa klabu ya Arsenal Alex Oxlade Chamberlain hatocheza kwa wiki kadhaa kutokana na jeraha la goti alilolipata jumanne wakati wa mechi ya  vilabu bingwa Ulaya.

Akiongea na wanahabari Kocha wa Arsenal Arsene Wenger amesema, Chamberlain alipata jeraha walipokabiliana na Javier Mascherano . Jeraha lake ni baya na litamuweka nje kwa wiki kadhaa,''alisema Wenger.

Chambaerlain mwenye umri wa miaka 22  aliondoka  katika uwanja wa Emirates akiwa na magongo.

0 comments:

Post a Comment

Want to comment? write down here