Pages

Sunday 24 January 2016

Mayanja aula mfupa uliomshinda Kerr


Dar es Salaam . Kocha wa Simba, Jackson Mayanja ameamua kucheza kamali iliyomshinda mtangulizi wake Dylan Kerr kwa kuamua kuwapa nafasi wachezaji Rafael Kiongera na Hassan Isihaka katika kikosi chake cha kwanza.

Kauli ya Mayanja imekuja wakati mashabiki wa klabu hiyo wakilalamikia kiwango cha Kiongera aliyerudishwa kwenye usajili wa dirisha dogo kuwa ni cha chini na hapaswi kupewa nafasi.

Isihaka amekuwa akilaumiwa kwa kushuka kiwango na mara kwa mara hunyooshewa kidole kuwa kuwa uzembe wake umekuwa ukiigharimu Simba.

Hata hivyo, Mayanja amedai kukoshwa na viwango cha wachezaji hao na ameahidi kuwa ataendelea kuwapa nafasi kwa sababu wanafanya kazi ambayo huwatuma.

Mayanja alisema haoni sababu kwa wachezaji hao kulaumiwa kwa sababu yeye kama kocha ndiye anayefahamu ubora na uwezo wa mchezaji mmoja mmoja kiufundi na siyo mashabiki.

“Isihaka amecheza mechi mbili mfululizo na hatujaruhusu bao na sioni tatizo lolote kutoka kwake.

Pia, Kiongera naamini ana kitu kikubwa kwa sababu anasaidia kuipeleka timu mbele sifa ambayo mshambuliaji anatakiwa kuwa nao.

Bado ni wachezaji ninaowaamini na wakiendelea kufanya vizuri nitazidi kuwapa nafasi,” alisema Mayanja.

Mayanja alisema kuwa falsafa yake ni wachezaji kuzingatia kile anachowaelekeza na yeye binafsi hawezi kuingia kwenye mkumbo wa kupangiwa kikosi na mtu yeyote<

 Charles Abel/Mwananchi

0 comments:

Post a Comment

Want to comment? write down here